
Kheri Ahmed Kombo
Mwanamuziki
MIMI NI NANI?
Mimi ni mwanaume. Natokea Pemba, nilizaliwa huko, katika kijiji cha Mwambani. Nina miaka 54. Nina familia, watoto sita. Mimi ni mwalimu. Tayari nimeshafanya mengi katika maisha yangu ya taaluma.
Jitazame kutokea mbali
Kwanza kabisa, unahitaji kujua wewe ni nani, ni mtu gani. Unahitaji kujifahamu.
Heshimu wengine na uheshimiwe
Kuheshimu wengine kunamaanisha kuwa na utu, kuwa mwanadamu. Kupenda na kupendwa. Usijihusishe na jamii zisizo nzuri, namaanisha waraibu wa dawa za kulevya au wezi. Tunapaswa kujijua sisi binafsi na kujua jinsi ya kuishi katika dunia hii. Fahamu watu wanapenda nini na hawapendi nini. Watu wanapaswa kuwa huru na kujiamini. Kama unataka kujua jinsi tunavyopaswa kuishi katika dunia hii, basi unapaswa kuwa pamoja na watu, kundi la watu walio wema. Watakufundisha jinsi ya kuishi.
Rithisha maarifa
Jambo la muhimu zaidi kwangu ni kurithisha maarifa niliyonayo kwa watoto wangu. Maarifa ambayo yanayoongelea kuhusu dunia: inakubidi kuwa karibu na watu, inakubidi uwashirikishe wengine kile ulichonacho.
Muziki unaoleta mabadiliko
Sauti ni maneno. Zile za ndani, na thabiti zinapoongelea huzuni na nyingine zinapoongelea furaha. Muziki ni lugha. Kwa kutoa sauti fulani, unazitengeneza. Zinaongea na wewe moja kwa moja kuhusu kile ulichonacho ndani yako, kwenye akili yako. Siwezi hata kuelezea kile ninachokihisi lakini nahisi kipo mbali sana ndani mwangu. Sauti hizi zinasafiri kwenye damu yangu. Daima nawaza kuhusu ngoma, natumia neno moja la Kiswahili ‘Nakupenda’. Nawaambia kwamba nawapenda. Ngoma ni kama tabibu. Kama mtu amefadhaika sana, ngoma ni kama dawa, zinaleta amani. Unapokuwa na hasira na ukaamua kusikiliza sauti za ngoma utajihisi vizuri. Sauti za ngoma ni mchezo wa ‘Mapigo ya Moyo’. Zinanifundisha maisha mazuri, maisha yenye upendo, zinanifundisha upendo. Zinafanya nafsi ijihisi huru, amani ya akili.
Nenda na mabadiliko katika dunia
Iwapo mazingira yanabadilika, dunia inabadilika, basi inakubidi ubadilishe namna yako ya kufikiri pia, hata kama jambo hili si sawa kwako.
Tengeneza maridhiano na wengine
Ni muhimu kuishi kwa namna inayoleta amani na mapatano kwenye mazingira yako. Amani na upendo ni mambo muhimu sana. Hata kama mtu ni mkorofi kwako, mpe upendo na amani yako.
–Je, inamaanisha nini kumpa upendo na amani? Unahitaji tu neno zuri, lugha inayoleta maneno mazuri. Mpe neno zuri. Muulize ‘Habari gani? Kila kitu ki sawa? Kwanza kabisa fahamianeni, karibianeni, changamkianeni mnaposalimiana, haijalishi kuna jambo gani kati yenu, kwa njia hii unaweza kuongea chochote kwa mtu huyo’. Subiri hasira iishe, nenda mbali kwa muda. Kisha rudi na ongea kwa utulivu. Tafuta maneno yatakayokutuliza. Tafuta suluhu ya jinsi ya kuishi nae kwa mahusiano mazuri. Ni kama umekutana na mbwa mkali huko mtaani. Ukikimbia, atakukimbiza, lakini ukisimama tuli, na usipokimbia, mbwa huyo naye hatakushambulia, na kila kitu kitakuwa sawa.
Samehe
Inakubidi ujisamehe mwenyewe, samehe mtu mwingine. Unapowaza mambo yale yale, hasa mambo mabaya, yatabaki kwenye fikra zako wakati wote. Tunapaswa kusamehe. Unaweza kupata nguvu ya kusamehe kwa kuzingatia unachokiamini, imani ya dini yako. Rejea siku za nyuma na mambo uliyopitia na yafuate. Jambo hilo litakupa suluhu.
Uwe na roho nzuri. Fanya maamuzi kwa ajili ya siku za usoni
Neno langu la mwisho ambalo ningependa kusema ni kwamba tunapaswa kuwa na roho nzuri. Tunapaswa kutafakari mambo yaliyopita katika muktadha wa yale yaliyotutokea. Tumeyapitia na kujifunza kutoka kwayo kwa ajili ya siku za uso