
Mariam Olban Ally
Mwalimu
MIMI NI NANI?
“Mariam Olban Ally katika umbo la kimwili amesimama mbele yako, lakini kiroho, ni “mtu fulani” angalipo (kicheko). Nilizaliwa kwa sababu fulani. Nina uhakika kuhusu hilo. Kwa sababu gani? Muda utaniambia kuhusu hilo.
Saidia watu
Furaha inaleta kuridhika kunakoeleweka si tu kama kutimiliza mahitaji binafsi, lakini pia kutimiliza mahitaji ya wengine, kikundi fulani, kuchangia furaha ya mtu fulani, kwa kutoa msaada. Huwezi kuwa na furaha kwa kuwa na furaha tu. Haiwezi kuwa rahisi hivyo. Ninapowasaidia watu, napata furaha. Nafurahi ninapojua kwamba namsaidia mtu na msaada huu ni wenye tija hasa. Hiki ndicho kinachoniongoza mimi kama binadamu. Sijui kama naweza kumsaidia mtu wakati wote, lakini wakati wote najaribu na wakati wote naamini kwamba naweza. Kwa njia yoyote ile, lakini naamini inawezekana. Wakati mwingine kijana hunifuata na kuomba pesa kwa kuwa hajala kifungua kinywa. Nadhani si vyema kutokupata kifungua kinywa na nampa shilingi elfu mbili. Nipesa kidogo lakini atapata kitu ambacho anakihitaji: kitu kidogo kitakachomfanya awe na furaha kulingana na fedha hiyo,
-Je, hii inamaanisha tunapaswa kuwapa watu kile wanachohitaji?
-Si lazima wakati wote kuwapa wanachohitaji. Muhimu ni kuwafundisha jambo fulani.
Dunia si kwa ajili yako tu. Unaishi miongoni mwa watu wengine
Dunia si kwa ajili yako tu, ila kwa ajili yetu sote. Daima tunaishi katika jumuiya fulani, unapaswa kujua inahitaji nini. Kama unaishi kwenye jumuiya, unapaswa kuelewa inataka nini. Watu wanaoishi ndani yake wanataka nini. Jumuiya yangu ni mahitaji yetu ya pamoja na jumuiya husika – “Tunategemeana”. Hatuishi peke yetu. Si mimi na familia yangu tu. Wapo wengine wanaonizunguka. Kuna jumuiya nyingine pia, na dini: Waislamu, Wahindu, Wakristo, na Singasinga. Hawa ni jirani zangu. Huwezi kuishi peke yako kwenye jumuiya. Jambo hili ni muhimu na ndiyo sababu tunapaswa kuelewana sisi kwa sisi na kufahamiana ili tuweze kuishi pamoja kwa amani. Sitaki kuibadilisha imani yako, na wewe vivyo hivyo hupaswi kuibadilisha imani yangu. Kama nitaenenda kwa mwenendo wa kawaida wa kibinadamu na wewe ukaenenda kwa mwenendo wa kawaida wa binadamu, basi hapo tutaishi pamoja kwa amani.
Sisi ni sawa. Umoja. Ufanano
Kuna lugha nyingi Afrika lakini katika zote kuna neno moja linalofanana la “utu”, “untu”, “mtu”. Maneno yote haya yanamaanisha kitu kimoja: “binadamu”. Kwa sababu sisi sote ni wanadamu, sisi sote tuna vitu vinavyofanana, mahitaji sawa, vitu vile vile hutuletea furaha, aina sawa ya maisha, na hata jinsi watoto wanavyokua. Sisi sote tunafanana kila mmoja wetu katika asili yetu ya ubinadamu na tunaongozwa na kanuni sawa za asili.
Kuza furaha. Furahia maisha
Kudumisha furaha ndani yangu, furaha ya nafsi, nadhani ndiyo siri ya kuwa na furaha. Hii ndiyo kanuni kuu ya furaha. Nafurahia maisha yangu. Maisha ni mafupi sana kwa kukasirika mara kwa mara au kuwa na huzuni, kutowapa watu tabasamu, kutowasalimu pale mnapopishana. Hayo mambo yanaleta raha.
Ishi maisha kikamilifu, kidhi mahitaj yako, na utakuwa tayari hasa kusaidia wengine
Nayakabili maisha jinsi yalivyo na naishi katika utimilifu wa maisha. Naufuata moyo wangu, ujana wangu. Nautunza moyo wangu wa ujanani, naulinda ndani yangu (kicheko). Kama nina mahitaji yoyote yale, nayakidhi. Kama nataka kwenda ufukweni, kwenda kanisani kusali, kukutana na rafiki – nafanya hivyo. Kwangu maisha ni kuishi maisha yenye utimilifu. Kuhisi kwa ukamilifu kile ninachokifanya. Kufanya ninachotaka kunategemea na muda na mahali nilipo. Nahitaji kuyahisi maisha na kutaka kitu fulani. Usiwe na mawazo, wakasirikie wengine au lalamika. Ninachofanya ni kujitazama, nini ni muhimu kwangu, nini nahitaji na nini nataka kukipata. Kwa njia hii nakuwa tayari kuwasaidia wengine pia. Bila ya kutosheleza mahitaji na hisia zako binafsi, huwezi kuwa tayari hasa kuwasaidia wengine.
Majibu ya maswali yanapaswa kutafutwa ndani yako mwenyewe
Kila mtu anapaswa kupata jibu la maswali yake. Kila mtu anapaswa kutafuta ufumbuzi wake, njia yake. Ninapoombwa ushauri, nasema keti chini, tafakari kwa kina, jiulize nini ni chema kwako. Hakuna mtu atakayekwambia jambo hilo. Unapaswa kutafuta jibu lako kwa ajili yako mwenyewe, ndani ya nafsi yako.
Kutumia muda pamoja
Hivi sasa watu wanaishi maisha ya kujitenga. Maisha yanakuwa “binafsi” sana kupitia vifaa vya mkononi, kuwa na iPads, iPhones na kompyuta mpakato. Maisha yanakuwa ya kujitenga mbali zaidi na wengine. Tunajifungia nafsini mwetu na ufaragha wetu. Hatuongeleshani, hatushirikishani. Tunatanga mbali na umoja wetu, hasa watoto na wazazi. Tunahitaji muda wa kuwa pamoja kijamii. Huwezi kuishi peke yako. Unahitaji kujichanganya. Una watoto, una familia, marafiki, una jumuiya yako. Unapopata tatizo, unapokuwa na mahitaji yoyote, unamhitaji mtu. Kisha unajua kwamba mtu fulani angalipo, kwamba mtu fulani atakuwa pamoja nawe. Kuwa peke yako … huwezi kuwa peke yako.
Kiasi. Kujidhibiti maishani
Kwa Kiswahili tunasema “Kiasi” yaani unapaswa kujidhibiti katika kula, kunywa, kuongea, katika kila kitu. Hatuwezi kujikita mara kwa mara katika kitu kimoja tu. Tunapaswa kujithibiti na kuwa na kiasi. Hakuna njia nyingine.
Wasaa. Wasaa ambao wewe upo
Ukweli kwamba nimekutana na wewe ni kwamba tumeketi hapa pamoja na kuongea – hili ni jambo muhimu. Hatimaye, mwisho wa siku, kile kinachonitokea mimi na kile kinachotokea hivi sasa ni jambo muhimu kwangu. Linanipa furaha.